NOVENA YA HURUMA YA MUNGU
KUHUSU HII NOVENA YA HURUMA YA MUNGU Hizi ni sala ambazo Bwana Yesu mwenyewe alimfundisha Mtakatifu Sista Faustina Kowalska. Bwana Yesu alimwambia: “Kwa Novena hii, nitazijaza roho za watu kila neema iwezekanavyo. Uisali daima rozari hii niliyokufundisha. Na yeyote atakayeisali Rozari hii atajaliwa kupata Huruma Kuu ya Mungu saa ya kufa kwake, hata wakosefu shupavu wakisali Rozari hii, hata kama ni mara moja tu, wataipata Huruma Yangu isiyo na mwisho. Kwa njia ya Rozari hii, unaweza kuomba chochote na utakipata, bora tu kipatane na mapenzi yangu. Ninataka dunia nzima iijue Huruma Yangu isiyo na mwisho. Nami ninataka kuwapa neema nyingi wale wanaoitukuza Huruma Yangu, hata neema zile wasizofikiria kuzipata”. Kwa kila neno moja la Novena hii, tone moja la Damu Takatifu hutoka katika Moyo Mtakatifu wa Yesu na kuidondokea roho moja ya mkosefu. “Heri mtu Yule ambaye katika maisha yake amejizoeza kuikimbilia Huruma ya Mungu, kwa maana siku ya Hukumu ya Mwisho hatahukumiwa. Huruma ya Mungu it...