Posts

NOVENA YA HURUMA YA MUNGU

Image
KUHUSU HII NOVENA YA HURUMA YA MUNGU Hizi ni sala ambazo Bwana Yesu mwenyewe alimfundisha Mtakatifu Sista Faustina Kowalska. Bwana Yesu alimwambia: “Kwa Novena hii, nitazijaza roho za watu kila neema iwezekanavyo. Uisali daima rozari hii niliyokufundisha. Na yeyote atakayeisali Rozari hii atajaliwa kupata Huruma Kuu ya Mungu saa ya kufa kwake, hata wakosefu shupavu wakisali Rozari hii, hata kama ni mara moja tu, wataipata Huruma Yangu isiyo na mwisho. Kwa njia ya Rozari hii, unaweza kuomba chochote na utakipata, bora tu kipatane na mapenzi yangu. Ninataka dunia nzima iijue Huruma Yangu isiyo na mwisho. Nami ninataka kuwapa neema nyingi wale wanaoitukuza Huruma Yangu, hata neema zile wasizofikiria kuzipata”. Kwa kila neno moja la Novena hii, tone moja la Damu Takatifu hutoka katika Moyo Mtakatifu wa Yesu na kuidondokea roho moja ya mkosefu. “Heri mtu Yule ambaye katika maisha yake amejizoeza kuikimbilia Huruma ya Mungu, kwa maana siku ya Hukumu ya Mwisho hatahukumiwa. Huruma ya Mungu it...

ROZARI YA MAMA BIKIRA MARIA

Image
Anza kusali Rozari kwa kuibusu miguu ya Bwana Yesu katika taswira (picha) yake Msalabani kisha fanya Ishara ya Msalaba ukiwa unasema “Kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu, Amina”.   Taja kwa ufupi nia za Rozari hii. Tangaza nia hizo kwa sauti kama mnasali wengi kwa pamoja, Mfano, “Tusali kuombea amani katika   1 ROZARI YA MAMA MARIA   nchi yetu na ulimwenguni kote, na tuunganishe nia hizo na nia zetu sisi wenyewe, nk) .           Baada ya Sala ya Nasadiki pamoja na ya Baba Yetu, tunamwomba Mungu (Utatu Mtakatifu) fadhila za Imani, Matumaini na Mapendo, zikiambatana na Salamu Maria tatu.   Mojawapo ya maneno yafuatayo huweza kutumika:   “Mungu Baba utuongezee Imani. Salamu Maria, …… Mungu Mwana   utuongezee matumaini, Salamu Maria, …… Mungu Roho Mtakatifu   washa nyoyo zetu kwa mapendo yako, Salamu Maria, …..” Au;   “Utuongezee Imani ee Bwana, Salamu Ma...