ROZARI YA MAMA BIKIRA MARIA
Anza kusali Rozari kwa
kuibusu miguu ya Bwana Yesu katika taswira (picha) yake Msalabani kisha fanya
Ishara ya Msalaba ukiwa unasema “Kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho
Mtakatifu, Amina”.
Taja kwa ufupi nia za
Rozari hii. Tangaza nia hizo kwa sauti kama mnasali wengi kwa pamoja, Mfano, “Tusali
kuombea amani katika
1
nchi yetu na
ulimwenguni kote, na tuunganishe nia hizo na nia zetu sisi wenyewe, nk) .
Baada ya
Sala ya Nasadiki pamoja na ya Baba Yetu, tunamwomba Mungu (Utatu Mtakatifu)
fadhila za Imani, Matumaini na Mapendo, zikiambatana na Salamu Maria tatu.
Mojawapo ya maneno yafuatayo huweza kutumika:
“Mungu Baba utuongezee Imani. Salamu Maria, …… Mungu Mwana
utuongezee matumaini, Salamu Maria, …… Mungu Roho Mtakatifu
washa nyoyo zetu kwa mapendo yako, Salamu Maria, …..” Au;
“Utuongezee Imani ee Bwana, Salamu Maria,…. Utuongezee
matumaini ee Bwana, Salamu Maria,…. Uwashe nyoyo zetu kwa
mapendo yako ee Bwana, Salamu Maria, …..” Au;
“Salamu e uliyechaguliwa na Mungu Baba, Salamu Maria,…..
Salamu e Mama wa Mungu Mwana, Salamu Maria,….. Salamu e
Mchumba wa Mungu Roho Mtakatifu, Salamu Maria,……”
Atukuzwe Baba, na Mwana
na Roho Mtakatifu, kama mwanzo na sasa na siku zote, na milele, Amina.
2
Ee Yesu wangu,
utusamehe dhambi zetu, utuepushe na moto wa milele, ongoza roho zote mbinguni,
hasa za wale wanaohitaji huruma yako zaidi.
Tuwasifu milele, Yesu, Maria na Yosef.
Kisha endelea na sala
zinazofuata kama mpangilio unavyoonyesha hapo juu.
Kila baada ya Tendo
moja na makumi ya Salamu Maria…, “Atukuzwe..”, “Ee Yesu wangu…” na “Tuwasifu
milele…” kama muda unatosha wimbo ufaao wa Bikira Maria uimbwe (kama muda ni
mfupi basi angalau ubeti mmoja mmoja uimbwe kila baada ya makumi hayo). Baada
ya Wimbo, Tendo linalofuata litangazwe kwa sauti pamoja na tafakari fupi au
ombi linaloambatana na Tendo husika kama inavyoonyeshwa hapa chini.
3
MATENDO
YA FURAHA (Jumatatu na Jumamosi)
Tendo la kwanza; Malaika
Gabrieli anampasha habari Maria kuwa
atakuwa Mama wa Mungu. Tumwombe Mungu atujalie unyenyekevu.
Tendo la
pili; Maria
Mtakatifu anakwenda kumtembelea Elizabeti.
Tumwombe Mungu atujalie mapendo ya jirani.
Tendo la tatu; Yesu anazaliwa Betlehemu. Tumwombe
Mungu atujalie
moyo wa ufukara
Tendo la nne; Yesu anatolewa hekaluni. Tumwombe
Mungu atujalie
usafi wa moyo.
4
Tendo la tano; Maria anamkuta Yesu hekaluni.
Tumwombe Mungu
atujalie kuwatii wakubwa wetu.
MATENDO
YA UCHUNGU (Jumanne na Ijumaa)
Tendo la
kwanza; Yesu
anatoka jasho la damu kwa ajili yetu.
Tumwombe Mungu atujalie sikitiko la dhambi.
Tendo la
pili; Yesu
anapigwa kwa mijeledi kwa ajili yetu.
Tumwombe Mungu atujalie kuacha dhambi za uchafu.
Tendo la
tatu; Yesu
anatiwa miiba kichwani kwa ajili yetu.
Tumwombe Mungu atujalie kushinda kiburi.
Tendo la
nne; Yesu
anachukua Msalaba kwa ajili yetu.
Tumwombe Mungu atujalie kuvumilia taabu.
Tendo la tano; Yesu anakufa Msalabani. Tumwombe
Mungu atujalie
kuwapenda Yesu na Maria.
MATENDO
YA UTUKUFU (Jumatano na Jumapili)
Tendo la kwanza; Yesu anafufuka. Tumwombe Mungu
atujalie kugeuka
watakatifu.
Tendo la pili; Yesu anapaa mbinguni. Tumwombe
Mungu atujalie kwenda
mbinguni.
5ROZARI YA MAMA MARIA
Tendo la tatu; Roho Mtakatifu anawashukia Mitume.
Tumwombe Mungu
atujalie bidii katika dini yetu.
Tendo la nne; Bikira Maria anapalizwa mbinguni.
Tumwombe Mungu
atujalie kufa vizuri.
Tendo la
tano; Bikira
Maria anawekwa Malkia mbinguni.
Tumwombe Mungu atujalie kudumu katika njia njema.
MATENDO
YA MWANGA (Alhamisi)
Tendo la kwanza; Yesu anabatizwa Mto Jordani.
Tumwombe Mungu
atujalie uaminifu kwa ahadi zetu za ubatizo.
Tendo la pili; Yesu anageuza maji kuwa divai huko
Kana. Tumwombe
Mungu atujalie kuukoleza ulimwengu kwa chachu ya enjili.
Tendo la tatu; Yesu anatangaza Ufalme wa Mungu.
Tumwombe Mungu
atujalie kupokea Ufalme wake kwa toba ya kweli.
Tendo la nne; Yesu anageuka sura. Tumwombe Mungu
atujalie neema ya
kuung’arisha ulimwengu kwa uso wa Yesu.
Tendo la tano; Yesu anaweka Sakramenti ya
Ekaristia. Tumwombe
Mungu atujalie neema ya kujitoa sadaka kwa ajili ya wengine.
6
· Bwana utuhurumie
· Bwana utuhurumie
· Kristo utuhurumie
· Bwana utuhurumie
· Bwana utuhurumie
· Kristo utusikie
· Kristo utusikilize
· Mungu Baba wa Mbinguni,…… Utuhurumie
· Mungu Mwana Mkombozi wa dunia ……… Utuhurumie
7
·
Mungu
Roho Mtakatifu …….. Utuhurumie
·
Utatu
Mtakatifu Mungu Mmoja …….. Utuhurumie
·
Maria
Mtakatifu ………. utuombee
·
Mzazi
Mtakatifu wa Mungu …….. utuombee
·
Bikira
Mtakatifu Mkuu wa Mabikira …….. utuombee
·
Mama
wa Kristo ……… utuombee
·
Mama
wa Neema ya Mungu ………….. utuombee
·
Mama
Mtakatifu sana ……… utuombee
·
Mama
mwenye usafi wa Moyo ……….. utuombee
·
Mama
mwenye ubikira ……….. utuombee
·
Mama
usiye na doa ……….. utuombee
·
Mama
mpendelevu ………. utuombee
·
Mama
mstajabivu ………. utuombee
·
Mama
wa Muumba ………. utuombee
·
Mama
wa Mkombozi ………….. utuombee
·
Mama
wa Kanisa……….. utuombee
8
·
Bikira
mwenye utaratibu ………….. utuombee
·
Bikira
mwenye heshima ………….. utuombee
·
Bikira
mwenye sifa ………….. utuombee
·
Bikira
mwenye uwezo ………….. utuombee
·
Bikra
mweye huruma ………….. utuombee
·
Bikra
mwaminifu………….. utuombee
·
Kioo
cha haki ………….. utuombee
·
Kikao
cha hekima ………….. utuombee
·
Sababu
ya furaha yetu ………….. utuombee
·
Chombo
cha neema ………….. utuombee
·
Chombo
cha kuheshimiwa ………….. utuombee
·
Chombo
bora cha ibada ………….. utuombee
·
Waridi
lenye fumbo ………….. utuombee
·
Mnara
wa Daudi ………….. utuombee
·
Mnara
wa pembe ………….. utuombee
·
Nyumba
ya dhahabu ………….. utuombee
9
·
Sanduku
la Agano ………….. utuombee
·
Mlango
wa Mbingu ………….. utuombee
·
Nyota
ya asubuhi ………….. utuombee
·
Afya
ya wagonjwa ………….. utuombee
·
Kimbilio
la wakosefu ………….. utuombee
·
Mtuliza
wenye huzuni ………….. utuombee
·
Msaada
wa waKristo ………….. utuombee
·
Malkia
wa Malaika ………….. utuombee
·
Malkia
wa Mababu ………….. utuombee
·
Malkia
wa Manabii ………….. utuombee
·
Malkia
wa Mitume ………….. utuombee
·
Malkia
wa Mashahidi ………….. utuombee
·
Malkia
wa Waungama dini ………….. utuombee
·
Malkia
wa Mabikira ………….. utuombee
·
Malkia
wa Watakatifu wote ………….. utuombee
·
Malkia
uliyepalizwa Mbinguni ………….. utuombee
10
·
Malkia
wa Rozari takatifu ………….. utuombee
·
Malkia
wa amani ………….. utuombee
·
Mwanakodoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia,…………..Utusamehe ee Bwana.
·
Mwanakondoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia,…………..Utusikilize ee
Bwana
·
Mwanakondoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia,…………..Utuhurumie.
·
Utuombee, Mzazi Mtakatifu wa Mungu,…………..Tujaliwe ahadi za Kristo.
Tuombe
Ee Bwana Mungu,
utujalie sisi watumishi wako afya ya roho na mwili siku zote; na kwa maombezi
matukufu ya Maria Mtakaatifu Bikira daima, tuopolewe na mashaka ya saa, tupate
na furaha za milele. Kwa Kristo Bwana wetu, Amina.
Comments
Post a Comment